HIZI NDIO BIFU TANO ZILIZOMSUMBUA SANA RUGE MUTAHABA WA CLOUDS FM.
Ruge
Mutahaba anaweza kuwa ametajwa kwenye masakata mengi ya ubaya dhidi ya
wasanii, akibebeshwa lawama kuliko mtu mwingine yeyote kwenye tasnia ya
muziki, lakini kwake ni mambo matatu tu ndiyo anaona yamemsumbua sana.
Mtaje
Mr ll, mtaje Lady Jay Dee na mtaje Q Chief, utakuwa umemkumbusha mbali
mkurugenzi huyo wa vipindi wa Clouds Media, ambaye pia amefanya kazi ya
kusimamia wasanii wengi na ndiye kiongozi wa chuo cha Tanzania House of
Talents (THT).
Katika makala haya, Ruge anazungumzia mambo
mbalimbali kwenye sanaa na kutaja migogoro mitatu ambayo hataisahau
tangu aanze kujihusisha na shughuli za burudani.
Endelea…
Swali:
Baadhi ya wasanii ambao waliwahi kufanya kazi na wewe wamekuwa
akilalamika mara baada ya kutoka katika uongozi wako, kwamba
uliwanyonya, walidhulumiwa na mengine mengi kuna ukweli kuhusu haya?
Ruge: Sidhani kama kuna mtu ambaye anaweza kusema jambo hivihivi. Mfano THT haina tofauti na chuo kingine.
Inatakiwa
uhitimu na uende. Ukiamua kuendelea kufanya mambo yako pale hukatazwi
na wala hakuna anayekufukuza, lakini lazima uondoke na wengine wapate
nafasi.
Sasa ukiona mtu ameondoka na kisha anashuka kimuziki ni
yeye mwenyewe ameshindwa kujisimamia.Nimefanya kazi na wengine wengi
kama kina Patricia Hilary ambao walifanikiwa kujenga nyumba zao. Iweje
starehe zako unilalamikie mimi?
Swali: Unadhani ni kwanini wanakutusi?
Ruge:
Nilichokigundua ni kwamba hawa wasanii wanaopita kulalamika huko
pembeni wanashindwa kujisimamia kutokana na mambo wanayoyafanya. Wengi
wao ni kama watoto wanatafuta pa kulilia hawapapati, wanatafuta mtu wa
kuongea naye lakini hawana.
Mwingine alisema anapata Sh40 milioni
kwa mwezi aliviambia vyombo vya habari kwamba kila wiki anatengeneza
Sh10 milioni, wewe mtu wa kupata hizo kwa mwezi ni wa kunilalamikia
mimi?
Sasa kama alipata milioni 40 kwa mwezi, kwa mwaka mzima
hukuwekeza usinilaumu. Jilaumu kwa sababu kwa mwaka ni Sh480 milioni,
mimi mwenyewe siwezi kupata faida hiyo kwenye biashara zangu.
Ninavyoona
waandishi wengi hawafanyi tathmini kuhusu hawa watu wanaolalamika, kuna
watu wakubwa ambao nilishawahi kufanya nao kazi, leo hii nikiwaitia
kazi wanakataa nisiwalipe fedha. Kuna kina Issa Matona, Bi Shakira,
Mwanahela, Patricia Hilarry mnawaangalia hawa au hao wengine?
Juma
Nature amemtukana Fella mara ngapi? Kina Keisha, MB Dogg wamemtukana
Tale mara ngapi? Mb Dogg alikuja na malapa hapa na wimbo wake wa
“Latifa”, Tale akaniambia tumsimamie huyu kijana.
Swali: Ni kweli kwamba wasanii wakiondoka katika usimamizi wanabaniwa katika vituo vyenu vya redio na sehemu nyingine?
Ruge: Ninarudi palepale hawawezi kujisimamia. Wengine wanachosahau ni kwamba walikosea hawakupata baraka.
Mwishowe
wanarudi na kusema kwamba walionewa, wanabaniwa kwa sababu ya mtu
fulani, si sahihi. Mimi mwenyewe napoona mtu anamtukana mwingine,
naangalia mpaka nakasirika.
Hii kitu ipo kila mahali sema ni
habari zaidi ikitokea kwenye muziki wa bongo fleva. Kwanini Clouds?
Mbona Mengi aliwapiga stop Ali Kiba na Ray C kwa sababu hakwenda kwenye
hafla ya walemavu, mbona haikuwa dili? Magic FM walimpiga stop Diamond
kwa miaka miwili?
Kwanini sisi tukiamua kwamba hatupigi wimbo wa
msanii fulani inakuwa ni ishu kubwa na ndiyo habari ya mjini? Kama ni
sera ya ndani ya Clouds, kwa nini Ruge Mutahaba anakuwa wa kwanza
kulaumiwa?
Swali: Ni bifu ngapi tano za wasanii ambazo zilikusumbua zaidi?
Ruge:
Mimi nimekuwa nikichukulia kama kunisumbua kwa sababu sijawahi kuwa na
bifu na msanii, lakini wao wanakuwa nazo kwangu. Nawashangaa watu wenye
mabifu. Mfano kwangu bifu lililonishangaza au kunisumbua ni lile la Anti
Virus.
Si
kwa sababu ya Sugu, bali wale waliomfuata. Kwa sababu kuna watu ambao
waliingia kiasi kwamba nikawa nashangaa hata walitokea wapi. Kwa sababu
nusu yao sikuwa nawajua ni kina nani.
Nilishangaa
ni kina nani ambao wanaweza kuingia kwenye ugomvi na mtu wasiyemjua?
Wapo katika maisha gani ya kuambiwa tu ‘gombana na mtu fulani’, na wewe
ukagombana na tena unatukana? Kilichokuwa kinanitatiza ni chanzo ambacho
(hao watu) hawakukijua na wala hawakutaka kukijua.
Na kwa sababu nilikuwa najua tatizo la Sugu, haikunisumbua. Tatizo ni hao wengine ambao sikujua wametoka wapi.
Kwangu
mimi sikuwa na ugomvi na mtu. Bifu ni kitu ambacho kipo pande zote
mbili. Kama kwako hauna bifu kunakuwa hakuna, labda kama upande wa pili
umeamua kuwe na bifu.
Ugomvi
wa pili ni dhidi ya Lady Jaydee. Ilikuwa ya ajabu sana kwa sababu
maneno mengi yalianzia mitandaoni hadi tukaamua kufungua kesi, ambayo
hadi leo haijaisha mahakamania. Kinachotakiwa sasa ni yeye kuomba radhi,
lakini mahakamani hatokei.
Haya
mambo ni bahati mbaya yalishatokea, kwa hiyo mtu yeyote akitaka kusema
jambo lolote lenye malalamiko lazima amtaje Ruge ili kitu chake
kijulikane zaidi.
Pia
Q Chief aliwahi kunitukana sana kipindi cha msiba wa Mangwea,
nikamfuata na kumwambia unanitukana, nitukane basi mpaka hamu yako iishe
nikiwa hapa hapa. Niliwahi kuambiwa kwamba nimezuia kibali cha
(mwimbaji kutoka Nigeria) Davido Basata, siyo kweli. Kwa bahati mbaya
najua vitu vingi.
Mtu
anaweza kufanya jambo akakataliwa Basata mimi nikaenda nikafanikiwa
akadhani kwamba nimembania, kumbe hajui sheria na mipaka ya Basata ni
ipi. na kwingine ni kupi.
Sisi
tulitaka kunyimwa kibali, tukawaambia Basata kwamba wakitunyima
tunakwenda mbele kwa waziri ndiyo utaratibu. Sasa mwingine akinyimwa
anadhani tumewabania.
No comments:
Post a Comment