Takriban wanawake
14 kutoka kisiwani Zanzibar nchini Tanzania wanaotuhumiwa kukiunga mkono
chama tawala cha mapinduzi CCM katika uchaguzi uliopita kinyume na
matakwa ya waume zao wamepewa talaka.
Kulingana na gazeti la Zanzibar daily Newspaper.Watalakiwa hao wamesema kuwa wanaume zao waliamua kuwapatia talaka nyakati tofauti kutokana na tofauti za kisiasa kwa mujibu wa gazeti hilo.
Limeongezea kwamba wanaharakati kutoka kwa muungano wa mawakili wanawake kisiwani pamoja na mungano wa wanahabari wa kike nchini Tanzania wamesikia kuhusu visa kama hivyo na wameahidi kufuatilia swala hilo.

No comments:
Post a Comment