Msanii
wa muziki kutoka Uganda, Desire Luzinda amefanikiwa kufanya onesho lake
la kwanza baada ya skendo ya picha za utupu, na kuweza kushangiliwa na
mashabiki tofauti na vile alivyokuwa anatarajia.
msanii wa muziki wa Uganda Desire Luzinda
Desire
ambaye picha zake za utupu zimeweza kumpatia wakati mgumu sana hasa
mbele ya hadhara, amewashukuru mashabiki hawa kwa kutoa shangwe kama
ambavyo wangefanya kwa mtumbuizaji mwingine yoyote yule, licha ya wakati
mgumu na wa aibu ambao amepitia.
Katika onesho hili la Desire mwishoni mwa wiki, shangwe za mashabiki ziliambatana na jitihada za kutaka kumsogelea karibu zaidi, malengo yao yakihisiwa kuwa ni kutaka kuhakikisha vile walivyoviona katika picha kwa uhalisia zaidi, huku wengine wakitafsiri kuwa hatua hii ilikuwa ni kuonesha upendo tu.

No comments:
Post a Comment